Tuesday, May 13, 2014

Mimi ni Polisi: Kisa cha Mke wa Waziri Part III

 Mimi ni Polisi: Kisa cha Mke wa Waziri

03/06/2011, Kituo kidogo cha Polisi Sekei

“Afande!” aliita askari aliyekuwepo nje ya kituo.

Nilitoka nje na kumuona dereva wa bodaboda akiwa ameshikilia mkono huku akionesha kuugulia maumivu makali. Pembeni kulikuwa na pikipiki yake ambayo kwa hali iliyokuwa nayo nilishangaa kama ni mkono wake tu ndio umepata tatizo.

“Afande, bodaboda huyu kagongwa amekujua kuchukua PF.3” Aliniambia askari yule.

“Duh! Alifanikiwa kushika hata namba za aliyemgonga kweli?” Niliuliza huku nikichukulia kuwa aliyemgonga alikimbia kwani katika wale watu waliokuwa wamemzunguka hakuna hata mmoja aliyeonekana kuwa na uwezo wa kumiliki gari.

Askari aliyekuwa naye aligeuka na kunionesha kwa kidole gari ambalo lilikuwa ndiyo linawekwa vizuri sehemu ya kuegesha magari huku sehemu ya mbele kushoto ya gari hilo ikiwa imeharibiwa kutokana na ajali hiyo.

Ilinibidi kumwagiza askari kumwandikia PF 3 haraka aende kutibiwa mapema na kuwaomba wale waliokuwepo eneo la tukio kama wataweza kubaki wachache niendelee kuchukua maelezo. Waliokuwepo eneo la tukio walianza kuniambia kuwa isingekuwa ustaarabu wa mwendesha gari, wangeshampiga tayari. Tukio lenyewe lilitokea katika makutano ya barabara za Arusha-Moshi na Waterfall. Mwendesha gari alikuwa akitokea kwenye barabara hiyo ya Waterfall akitaka kuingia kwenye barabara kuu ya Arusha-Moshi ambayo mwendesha pikipiki huyo alikuwa akiitumia.

Kabla hawajamalizia kunielezea mkasa mzima ....



Itaendelea...

No comments:

Post a Comment