TABATA
October
06, 2009 Siku ya Jumanne.
Background:
Nilikuwa nimemaliza zangu chuo
MUCCoBS kozi ya BAF na kufanikiwa kupata GPA nzuri tu ya 4.2. Nilikuwa na
matumaini na ndoto nyingi za mbeleni juu ya maisha yangu. Nilipenda sana elimu
na nilitegemea kupata nafasi ya TA (Tutorial Assistant) chuoni hapo. Wakati nangojea graduation ambayo huwa mwezi November, nilikuja Dar es salaam kumtembelea dada yangu ambaye alikuwa akiishi huku, Tabata! Naye ndo kwanza alikuwa na mwaka mmoja kazini ila kwa bahati (nzuri?mbaya?...sijui) alipata uja uzito na mshkaji mmoja hivi walisoma naye chuo.
Basi nikawa nakaa naye pale huku nikingojea siku zisonge.
October
06, 2009 siku ya Jumanne:
Siku hii alitakiwa kwenda clinic na
kwa vile alikuwa karibu sana na kujifungua hakuweza kuendesha gari ikabidi
nimsindikize kwenye zahanati moja pale Tabata nimeisahau jina.
Basi wakati namngojea nikaenda
kukaa kwenye mabenchi Fulani pembeni pale kuangalia TV. Karibu yangu alikuwa
amekaa binti mmoja mrembo sana kwa kweli. Sikufahamu yupo pale kufanya nini.
Nilidhani na yeye kaja kumsindikiza ndugu yake labda.
Mimi bila hiyana nikaacha kuangalia
TV nikaanza kupiga stori za hapa na pale. Tukakonekt vizuri na kuchangia
changia mada iliyokuwa inaonyeshwa kwenye TV. Baada ya kama nusu saa dada naye
akatoka ndani akaja tuondoke. Nikamwambia dada kama hutojali unipatie namba
yako tuzidi kuwasiliana.
Baada ya siku ile tuliendelea
kuwasiliana sana tu. Tulikuwa tuna chat mpaka ma saa sita ya usiku na
ukizingatia sikuwa na kazi. Aliniambia yupo chuo mwaka wa tatu anasoma Sheria.
Moyoni nilihisi hapa nimepata mtu
lakini kama nilivyofundishwa sikuwa na papara ya kumtamkia hayo. Bado
ninakumbuka maonyo niliyopewa juu ya jiji hili la Daslam!
Baada ya wiki mbili hivi tulikutana
for lunch posta..enzi hizo break point bado mpya kabisa. Tuliongea mengi about
life.
Tabata:
Wiki moja kabla ya graduation
nilimwambia naenda zangu Moshi wiki ijayo hivyo ningependa tuonane. Alikubali
na kuja Tabata jioni. Tulikaa tukala na kupiga stori mpaka mida kama saa sita
ivi. Nikatumia mbinu za medani za kivita kumshawishi kwamba kwenda hostel kwao
mida hiyo ingekuwa ngumu ilhali tungeweza kuchukua tu chumba hapo asubuhi arudi
chuoni. Of course, strawberry lips na contessa vilichangia kunisaidia kumfanya
akubali. Ila alikuwa amekataa sana mwanzoni.
Tulienda guest moja inaitwa MUNGU
ANAKUONA GUEST HOUSE & RESTAURANT. Nikalipa, tukaingia ndani.
Kazi ikaanza kuomba game ila haikuwa
ngumu…long liiive govinder kumar! Basi purukushani za hapa na pale za kujiandaa
na game na mimi kwa kuwa nilichanganya Contessa gin na White horse nikasahau
kabisaaa matumizi ya kinga.
Nikaenda zangu graduation November
na kurudi. Nikawa nimempotezea kabisa Yule binti kama ilivyo kawaida yetu baada
ya kupata tunda.
Jana,
March 17 2013 Jumapili:
SMS: “Ndugu yangu, kama umenichunia
sawa ila mbona hata sikuoni tena hospitali?”
Nikashtuka hospitali? Si ikabidi nimpigie!!!
Ananiambia: “Si pale Tabata sikuoni ukija tena kuchukua ARVs”
Conclusion:
Kumbe benchi nililokuwa nimeenda kukalia ile siku lilikuwa la
wagonjwa wa UKIMWI na yeye alikuwa akisubiri kuchukua dawa.
Mimi nikamwambia acha kunidanganya mbona wewe unaishi hostel
Kigamboni na ninajua hivyo..yani huko kote hakuna dispensary?
Akaniambia wagonjwa wengi hawaendi kuchukulia dawa karibu na
kwao kwa kuhofia kunyanyapaliwa hivyo alijua na mimi nipo kwenye foleni ya
kuchukua dawa ndiyo maana hakuona umuhimu wa kunilazimisha kutumia kinga.
Nilishtuka...nikazimia…ndo nimeamka leo...
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
No comments:
Post a Comment