Sunday, December 29, 2013

Vita vya Tatu vya Dunia...

VITA VYA TATU VYA DUNIA

Kama ilivyo kwa wanawake, inapokuja kwa wanaume, mwanamke pia anapata pointi au kupunguza pindi afanyajo jambo, LOLOTE LILE. Na ‘HAPATI POINTI’ yeyote kwa kufanya lile lililo bayana yeye kufanya, au lifahamikalo kama wajibu wake.

MFANO:

Kupokea SMS (-5) ~Kupokea SMS siku zote (isiyotoka kwangu) hupunguza pointi.
Imetoka kwa mshikaji wako wa zamani (ex) (-50), anakuita ‘mpenzi’ (-150); anataka mkutane (-80); kwa chakula cha jioni (-200); Serena Hotel (-300); Ijumaa jioni (-6000).

Sawa, umekubali tuangalie movie...action movie (+50); unauliza maswali kila dakika (-20); unaongelea jinsi DENZEL WASHINGTON alivyo mzuri (-50); unasifia zaidi kifua chake (-100); unaacha kuongea (+200); unalala (-500).

Unakubali kunisindikiza kwenda kuangalia mechi ya SIMBA na YANGA Uwanja wa Taifa (+100); unavaa jezi ya YANGA (+200); ila unaivua kufutia siti (-50); unakaa na mimi muda wote wa mechi (+60); ila unaondoka kwa muda kidogo (-20); kwenda kumsalimia rafiki (0); anaitwa Alfred (-500); Alfred anaendesha CELICCA (-6500).

Unapika (0); chakula nikipendacho (+70); chakula ukipendacho (-50); unatumia masaa manne kumaliza kupika (-50); unapika huku ukiwa whatsapp (-100); una chat na Aggrey Kimaro (-20,000).


Kujibu SMS zangu (0); kwa wakati (+10); jibu lenyewe ni kaherufi kamoja (-50); unatumia neno  ‘K’ kwenye majibu yako (-500); nakuuliza ulipo unajibu, “nimetoka na marafiki zangu…” (-200); mmeenda Akemi restaurant (-80); ni marafiki wa kiume, eti ulisoma nao chuo (-800).

Unaenda saluni (0); unaweka ‘weave’ (-75,000).

Tunatoka (0); tunakaa pamoja muda wote (+80); ukinywa zanzi (0); mpaka sasa umeshakunywa viroba nane (-60); na unataka vingine vinne (-150); unaamka kucheza (0); unacheza staili ya ‘bend-over/twerking’ (-90); kwa mshkaji anaitwa Arnold (-200); unarudi lisaa limoja baadaye (-80); bila ‘bra’ (UFOO-SARO).

Unafuatilia mazishi ya Kanumba (0); unamsikitikia Lulu na wafiwa wote (0); na kushukuru walau alitoa mchango kwa tasnia ya muvi tanzania (+10); alikuwa mwigizaji bora kwako (+2); unakaa masaa kuangalia picha yake (-80); unagusa TV ukijaribu kugusa uso wake (-200); unatamani wakati wa uhai wake ungekutana na Kanumba (-600); au umpate mwanaume kama yeye (-5000).

Ukijamba (-100) tena (-500).

Umeenda kanisani (0); na Biblia (+100); ukakaa nyuma kwenye kona (-60); ukiegemea ukuta (-80); Biblia umeiweka juu ya uso wako (-100); Unakoroma (-500).

Umekubali kufanya mapenzi (0); umejilaza tu (-600); bila kufanya chochote (-1000); tena bila kutoa mguno wowote (-500); unauliza kama imeshaingia (-6000); na kushituka nikikuambia kuwa tayari nshaingiza (-7000); unauliza kama nshamaliza (-8000); unaanza kuchat na rafiki yako (-9000); katikati ya tendo (-60,000); rafiki mwenyewe anaitwa Jeffrey Jessey (-10,000); Jeff ni mwanamitindo (VITA VYA TATU VYA DUNIA).

No comments:

Post a Comment