Saturday, September 7, 2013

Mke wa Pili

Mke wa Pili

18 August 2013, Sunday

Jumapili nilienda kwenye msiba wa mke wa jirani yangu, Alfred.

Kama kawaida nilikuta watu wamekaa kwenye vikundi vikundi kulingana na rika na kuzoeana. Ila mimi kwa utundu wangu wa kupata hadithi na busara za wazee nikaona nijongee panapo wazee. Walikuwa kama wazee sita.

Nilipofika nikawakuta wakiongea kuhusu hali ya jirani yetu huyo, bwana Alfred. Kwa kweli tangu msiba wa mkewe hakuwa katika hali nzuri. Kwanza ile tu kuambiwa “Mkeo amefariki” alianza kwa kuangusha kilio na kugaragara sana. Hadi wakati huo wa msiba, siku tatu baadaye bado hakuwa katika hali nzuri.

Ndipo mzee mmoja akawa anaongea kuwa wao huwa hawana shida sana wanapoletewa taarifa kama hizo kwani mpaka aje kuambiwa ni mke yupi kafariki presha ishashuka.

Ilikuwa kama hivi; (let’s say huyo mzee anaitwa mzee Chande)

Mzee Chande: “Dah! Yani Fredy kuambiwa tu mama Ana kafariki keshaangua kilio na kuzirai. Sisi bwana huwa hatuna hiyo shida”
Mzee John: “Unamaanisha nini Mzee Chande hapo?”
Mzee Chande: “Ahaha..yani mimi akija mtu akaniambia ‘Mkeo kafariki’ wala sina presha. Naanza kuuliza mama Asha, mama Amina, au mama Anifa?”
“Mpaka aje kunitajia ni mama Amina mimi presha ishashuka.” Alimalizia Mzee Chande.
Mzee John: “Ila bwana Chande wewe mbona sisi tunajua una mke mmoja bwana unatufunga kamba sisi. Ulioa lini wewe?”
Mzee Chande: “Ninao watatu kwa taarifa yako.”
Mzee John: “Ilikuwaje kuwaje aisee mpaka ukaoa tu mke wa pili?”
Mzee Chande akacheka kidogo na kukohoa kusafisha koo huku akionekana kukumbuka jambo la muda mrefu…
Mzee Chande: “Ndugu yangu, unajua nilishawahi kukaa mwaka mzima bila huduma yangu ya ndoa wewe?”

‘Aaah wapi’, ‘acha kutibia’ ‘haiezekani’ wote tulidakia kwa maneno tofauti kuonesha kupinga usemi wake huo.
Mimi mwenyewe nilijitafakari pamoja na kuwa single lakini sijawahi kupitisha mwaka …nikajua hapa tumeibiwa.

Mzee chande: “Ahaha mbona mnabisha, sijamaanisha kuikosa kabisa, ni kutoka kwa mke wangu tu.”
Mzee John: “Enhee hebu tueleze ilikuwaje”
Na mimi nikajiweka kitako vizuri kujifunza jambo…Mzee Chande akaanza simulizi.


28 January 1994, Ijumaa

Huyu Asha mnayemwona na mdogo wake ni watoto wa mke wangu wa kwanza. Baada ya kuwa tumeshaoana miaka kama sita hivi ghafla siku moja narudi nyumbani tumefanya shughuli zote za jioni, tukapata mlo wa jioni vizuri tukaenda kulala. Huko ndiko nikapatwa na mshtuko kwani nilipojigeuza na kumpapasa mama Asha, namkuta kavaa kibukta cha jeans.

Nikaguna nikainua kichwa kuthibitisha nilichoshika ni chenyewe kweli au la. Ni kweli bwana alikuwa kavalia kipensi cha jeans kajigeuza upande wa pili. Wala sikumsemesha nikajigeuza na mimi nikalala. Kichwa nilibaki na maswali mengi sana kwa nini? Si angeniambia tu kachoka? Au yuko siku zake? Lakini hapana si wiki jana tu kamaliza mzunguko? Kwa kweli nilikosa jibu.

Walisema ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Kweli hali ile iliendelea siku hadi siku, wiki, na miezi. Nikimuuliza ananiambia kachoka, hajisikii na vijisababu vingi tu. Kwa kweli kuna nyakati ilinibidi ‘kumbaka’ kwani hamu ilinizidi na sikuwa na njia mbadala.

Baada ya kama miezi sita nikakutana na dada mmoja (ambaye ndo mama Amina) akawa amenivutia na kwa miezi hiyo iliyobaki nikawa napunguza uchovu kwake. Kwahiyo nikitoka kazini mimi huyooo kwa dada yule then ndo narudi nyumbani. Akijigeuzia ukutani mimi najigeuzia mlangoni. Ila sikuacha utaratibu ule wa kumpapasa lest awaze kuna mahali ninapata pumziko. Na kila wakati alikua amevaa kipensi chake cha jeans.

Baada ya mwaka kukatika nikamfuata mke wangu na kumwambia, “Mama Asha, nataka kuoa mke wa pili”
Mama Asha: “Oa!”
Nikamwambia, “Sawa basi mwezi ujao nitamua Latifa binti Omari”
Mama Asha, “We si uoe bwanaa!”

Basi mimi nikafanya maandalizi pale na kwa kuwa nilikuwa nimeshajipanga basi kila taratibu zikawa zimekamilika ndani ya mwezi huo huo mmoja.
Siku moja kabla ya harusi nikamwambia mke wangu nguo hizo hapo kesho ndo siku yenyewe. Akanikatalia kabisa kwenda, akaniruhusu tu kwenda kuoa.

Basi nikaenda kuoa mke wangu wa pili, March 1995, 31st siku ya Ijumaa. Ndugu wa mke wangu walikuwepo kwenye harusi hivyo walishuhudia na kuhakikisha vyote vimeenda kama ilivyotakiwa especially walitaka kuhakikisha kuwa yule dada anajua kuwa anaolewa (mpari) yaani mke wa pili.
Basi kama ada nikatumia siku zangu tatu kwa mke wangu mdogo na ya nne nikarudi kwa mke mkubwa.

Jioni kama kawaida tumejilaza nikaanza kumuuliza habari za nyumbani na nini.

Akanijibu kote salama. Nikamuuliza, “Unga upo?” akanijibu “upo”. Vivyo hivyo kwa mchele na sukari na yale mahitaji makubwa. Basi nikamwambia hebu nyanyuka kwenye suruali yangu pale kuna kama laki na nusu hivi utatumia kwa vitu vingine vidogo vidogo since umeniambia mahitaji mengi bado yapo.

Akanyanyuka na ghafla nikamtupia jicho nikaona kavalia upande wa khanga peke yake, na si unajua ugonjwa wangu mzee John, sichagui mamodo mimi. Basi kila kitu kinajitingisha nikiona. Akachukua zile fedha na kurudi kulala.

Nikazima taa na kujigeuza zangu uelekeo mlangoni kama ada. Hazikupita dakika kumi nashangaa upaja huu juu yangu. Yaani alikuwa wa moto balaa. Na mim…wazee wenzake wakaanza kupiga kelele za ‘ayaaa kajilengesha mwenyewe’ ‘usiniambie ulikula mzigo’ ‘yani hapo ndo unamwacha hanging kabisa’ nk nk…”Subirini nimalizie sasa wakubwa.”

Basi mimi nkampa haki yake pale tukalala. Miezi miwili mitatu baada ya pale akaniambia hataki ndoa ya mpari. Katika kuchunguza nikaja kugundua ushauri huo amepewa na dada yake ambaye ni msambe na ana watoto watatu wa baba tofauti. Nikamuambia mwenzangu wewe, unapokeaje ushauri kutoka kwa mtu ambaye hata ndoa haijui? Akang’angania kabisa. Basi nikamuambia nenda nyumbani ukatafakari suala hilo kabla hujafikia uamuzi wa mwisho. Kumbe lilikuwa kosa kwani huko ndiko alikoenda kujazwa uongo na dada yake, huyo msambe.

Akanipigia simu akaniambia nipe talaka yangu mimi sirudi tena. Nikamwambia nirudishie wanangu nikupe talaka yako. Tulibishana kwa muda kuhusu suala hilo la watoto.

Ikanibidi kufika nyumbani kwao kabisa na kukaa kikao na wazazi ndipo wakamwambia kama anataka talaka hana budi kuniachia watoto. Hapo ndipo tukakubaliana nikamwandikia talaka yake na kesho yake nikarudi nyumbani na wanangu.

Baada ya mwezi mmoja mke wangu mdogo akahamia kwangu kabisa.

Mara ghafla tukasikia watu wakiimba kuashiria kuwa muda wa kwenda makaburini umefika. Hivyo tukakatisha stori pale na kuelekea kunako kilichotuleta. Nasikitika tu sikupata wasaa wa kumuuliza Mzee Chande (baba Asha, Amina na Anifa) kwa nini alioa mke wa tatu…labda nikirudi tena kijijini huko nitamuuliza.

Wasalaam wapendwa,
Mentor.

No comments:

Post a Comment