MAMA PRINCESS
Disclaimer: Majina na mahali palipotajwa humu ndani havina uhusiano na watu ama mahali pa kweli. Ni vya kutunga…17th May 2013, 17:40..nikitoka ofisini
Rafiki yangu Cedrick alinipigia simu na kuniambia twende zetu samaki-samaki town campus (ndivyo tunavyoiita samaki2 ya posta.) Nikamwambia najisikia kuchoka sana tulikuwa na vikao vingi hivyo nataka kwenda tu nyumbani kupumzika.
Kishawishi cha kwenda kushinda pale samaki nikawa nimekiepuka. Nikaendesha zangu gari kuelekea nyumbani, Kigamboni.
Kwa kweli nilikuwa nimechoka na hata hamu ya kupika sikuwa nayo. Hivyo nikajilazimisha kwenda kununua chips maeneo Fulani ya kule home (tunapaita sebuleni). Nikapaki gari nje ya kibanda nikashuka kuelekea kaunta kuagiza.
Nikamuona mtoto mdogo amekalishwa kwenye kaunta pale…kabla sijamtupia mamaye macho nilivutiwa kwanza na uzuri wa mtoto Yule. Ni kashombe flani ivi..kazuri! Yani ni wale unawaangalia unawaza, ‘huyu akiwa mkubwa atawasumbuaje kina KakaKiiza wa enzi zake!!!!’
Basi mentor nikaanza kukachokoza pale na kukatekenya nikakanyooshea mikono kakakubali kubebwa. Nikakabeba kanacheka…
Nikaanza kumvutia picha mama yake atakuwaje kama katoto kake kazuri namna hii! Ndipo nikatupa macho upande alipo mama yake. Binti mdogo tu shombe shombe na yeye…mzuri kwa kweli! Yani ni mzuri mpaka nikakasirika kujua ndiye mama wa Yule mtoto niliyembeba. Ndiyo nilisikitika kwani ningetamani binti Yule angekuwa licha ya kuzaa awe hajaolewa kabisa..ningefurahije Mentor mimi!
Mentor: “mh! Wewe ndo dada yake huyu mrembo?” (kimoyomoyo nikitegemea aniambie ndiyo)
Mama Princess: “Hahaha..mimi ni mama yake, anaitwa Princess”
Mentor: “Mh mama Princess..kwenu ni wazuri hivi au ni wewe tu?” (Mama Princess akacheka)
Mentor: (huku nikijifanya namuongelesha Princess sasa) “Mama Princess hana mdogo wake mwingine kweli?”
Mama Princess: “Na yeye ameshaolewa!” (unaweza pata picha nilivyovunjika moyo)
Mentor: “Basi itabidi nimngoje Princess mwenyewe mpaka akue”
Mama Princess: “Na kweli…”
Basi tukaendelea kuagiza vilivyotuleta pale huku nikiendelea kucheza na mchumba wangu mpya, Princess.
Baada ya kuchukua vyakula vyetu nikamwambia mama Princess anioneshe Princess anapoishi nije kumtembelea mchumba wangu! Ila kwanza nikauliza kama baba Princess yupo ili nijihami kabisa. Akasema baba Princess hakai pale…(watu weweeeee!!!!!!)
Kusema kweli kwa wakati ule sikuwa nimetilia mawazo sana kwa mama Princess..ila majaribu yanavyokuja bana! Acha tu…Basi mama Princess akanionesha wanapoishi nikamwambia waingie kwenye gari niwasogeze pamoja na kwamba muda wa kuingia kwenye gari ungetosha wao kutembea kuelekea kwao.
Akaingia kwenye gari akanipa na namba ya simu kabla ashuke nikaisave Princess kabisa kumuonesha kuwa lengo langu ni mchumba wangu mpya, Princess.
Nikarudi zangu nyumbani nikaendelea na ratiba nyingine nikajiandaa kulala. Mida kama ya saa nne mama Princess akanitumia ujumbe mfupi kuwa Princess analala ndipo nikakumbuka kumbe ninatakiwa kusema usiku mwema kwa mchumba!
Nikapiga simu akapokea mama mtu kwani Princess mwenyewe hana zaidi ya mwaka mmoja. Tukapiga stori kidogo pale akaniambia baba Princess yupo ila mtu wa mishe sana nikasema haina shida nitakuwa nakuja kuwaona mara moja moja tu!
Nikawatakia usiku mwema…ikawa usiku ikawa asubuhi siku ya kwanza.
18th May 2013, 08:23am..Jumamosi
Baada ya kufanya usafi wa nyumba na mazingira kidogo nikasema niende kununua mkate ninywe chai ndipo tujue utaratibu mwingine wa siku. Nikatoka hivyo hivyo na vest yangu kuelekea dukani ambako ni njia hiyo hiyo ya kwa mama Princess. Nikanunua mkate wangu na maziwa, Tanga fresh packets mbili. Wakati narudi nikapitia kwa mama Princess nikampigia simu kujua kama ameshaamka akasema yupo macho nikamwambia afungue mlango kwani nina mzigo wa mchumba wangu.
Alipotoka nikamkabidhi maziwa yale akanikaribisha ndani kuwa ndo mchumba wangu ameamka muda huo. Kishingo upande na uwoga mwingi nikaingia ndani wanapoishi baba na mama Princess. Nikambeba Princess pale ikabidi nikabidhi na mkate wangu apike chai tukanywa wote pale huku tukiongea mawili matatu.
Katika kuongea akajikuta anafunguka kwangu kuwa yeye na baba Princess kwa siku za karibuni hawakuwa katika hali nzuri haswa baada ya yeye kujifungua. Amekuwa mtu wa kwenda nje sana na kurudi usiku (tena akiwa kachoka). Kuna nyakati anaweza kumpiga kabisa kisa kitu kidogo kama kusahau kuzima taa asubuhi n.k. (sijawahi kumuelewa mwanaume anayempiga mkewe..BUT hiyo ni topic ya siku nyingine)
Mambo haya yalijitokeza sana baada ya mama Princess kujifungua. Lakini, bado alivumilia. Nilishtuka kujikuta ni saa 10:56am. Ikabidi nisingizie kuwa sikufunga mlango kwangu nikaondoka.
Ikawa jioni ikawa asubuhi siku ya pili.
26th May 2013, Jumapili
Tuliendelea kuwasiliana na mama Princess kupitia simu na kumjulia hali mchumba wangu kila nilipopata nafasi.
Jumapili hii nilikuwa naelekea zangu beach, Majaribu beach, nikamwambia mama Princess kama vipi twende wote tukaogelee. Akaniambia atakuwa ameshasahau. Nikamshawishi akanikubalia na kwamba anegkuja na mchumba wangu kabisa. Basi jioni ile nikawapitia tukaelekea beach.
MH! Mama Princess…ni binti ambaye kama asipokuambia ana mtoto wala huwezi kudhani…kigoli haswaaa!!! Sasa pata picha kava bikini. Mama Princess kwa kweli alinitia majaribuni. Ila nikajisahaulisha na kujiambia mke wa mtu huyo..hata kama hawana ndoa..kuna mtu anahudumia tayari, kuna mtu keshamzalisha..alimuona kabla yangu..niwe mpole.
Ukweli ni kuwa, nilijitahidi kujipa sababu za kutomuwazia maovu mama Princess ila nilishindwa. Kila nikijisemea kuwa ni mke wa mtu akili yangu inaanza nayo kujibu angekuwa mke wa mtu si mwenye angemheshimu basi, angemtunza kama mwanamke..na tena si mwanamke tu, mwanamke mzuri na mama wa mwanaye!
Tuliogelea pale na kukimbizana hapa na pale na jua lilipotua tukarudi nyumbani…Tulipofika akanikumbatia na kuni ‘peck’ shingoni kusema asante.
ikawa jioni ikawa asubuhi siku nyingine.
Tuliendelea kama kawaida kuchat na mama Princess kwa simu na tuliongea mengi sana kuhusu changamoto zake na baba Princess.
Alinieleza jinsi ambavyo baba Princess amekuwa akikwepa majukumu mengi ya nyumbani na kuishia kuyafanya yeye mwenyewe. Ni bahati kwake kuwa anafanya kazi. Na mbaya zaidi ni jukumu lile kubwa kuliko yote. Hata wakilifanya, hakuwa akifurahia tena. Wanafanya pale tu baba Princess akitaka.
Basi mimi nikajifanya mkwe msamaria mwema nikawa namtia moyo na kulaani vitendo vya baba Princess. Nikamwambia, binti mzuri kama yeye, mama wa mwanaye hana haki ya kutendewa vile. Akawa anafurahi sana kuwasiliana nami.
31 May 2013...another Friday
Ijumaa hii mama Princess aliniambia nikirudi kutoka kazini nipitie kwake atanipikia. Nikajiambia bahati si ndiyo hii! Nikamaliza kazi zangu mapema tu kilichonichelewesha ni foleni ya kungojea pantoni (sijui daraja litajengwa lini jamani).
Nikafika home faster nikachange na kurudi kwa mama Princess mida ya 19:40. Nikakuta ndo anamalizia kuunga mchuzi wa samaki. Kaweka kasongi cha ‘Buy Me a Rose’ kwa sauti ya chini kanatumbuiza huku na yeye akikifuatisha kwa ku-hum.
“Buy me a rose,
Call me from work,
Open the door for me what would it hurt,
Show me you love me by the look in your eyes,
These are the little things I need the most in my life.”
Tusiongelee chakula…ila kilikuwa kinanukia na kitamu. Wahenga
walisema, ‘the way to a man’s heart is through his stomach.’
Nikajiuliza, inakuwaje baba Princess hajaingiwa moyoni bado? Au ni hulka
yake tu. Kilikuwa kitamu chakula kile bana…utani pembeni. Call me from work,
Open the door for me what would it hurt,
Show me you love me by the look in your eyes,
These are the little things I need the most in my life.”
Nikikumbuka jinsi ilivyoanza nitawaambia ila nilishtuka ni 22:33 na nipo juu ya mama Princess. Alikuwa anahema kama mtetea aliyekimbizwa na majogoo mawili. Asikuambie mtu…(na hii sisemi kujisifia) mama Princess ni mtamu balaa! Ni zaidi ya wali samaki alionipikia. Anayajua mautundu..na kujikunja…kifupi, sikuona bado tatizo lake. Nilikuwa kwake kama mwanafunzi mtiifu na yeye mwalimu aliyebobea akiitikia kila nikijibu swali…akahitimisha na machozi ya furaha baada ya kumaliza kusahihisha mtihani ule.
Sikuwa na muda wa kujiuliza nini kimetokea nikanyanyuka na kukusanya vilivyo vyangu na kurudi kwangu.
Ikawa usiku ikawa asubuhi kosa la kwanza.
02nd June 2013, Sunday
Wahenga walisema, “Kutenda kosa si kosa; kosa ni kurudia kosa!” Niliwaza utamu ule wa juzi ulioniingia hadi utosini nikajiambia kuna wanaume hawajui walitakalo maishani. Utakuwa unatafuta nini tena ukiwa na mama Princess? Licha ya kwenda nje tu..atakuwa amekukosea nini mpaka unyanyue mkono wako umpige kama si laana za kwenu!?? Alikuwa almost the perfect package (nasema almost kwa sababu tu hakuwa wangu).
Nikamtumia ujumbe mfupi kumjulia hali na kuomba samahani kwa yaliyotokea juzi. Akaniambia nisiwe na wasiwasi na anashukuru kwani ana muda mrefu hakuwa amejisikia kama mwanamke.
Jioni ya siku ile nikaenda tena…ikawa usiku ikawa asubuhi muendelezo wa kosa.
Ikawa ndo tabia yangu (yetu?) nikitoka kazini napitia kwa mama Princess (yeye alikuwa akitoka mapema sana kuja kunyonyesha mtoto..wanajua wenyewe arrangements zao).
Kuna siku baba Princess alikuwa akirudi nikawa nakasirika kimoyomoyo halafu ananitumia ujumbe nisijali kalala wala hakitumii!
Tuliendelea hivyo tukahamishia mchezo wetu kwangu nikawa namwachia funguo kabisa. Kiasi kwamba nikirudi anakuwa keshapika na kusafisha nyumba basi mi ni kupakua tu…vyakula vyote!heheh…
Fast forward…August 2013
Wiki ya mwisho ya mwezi wa saba mama Princess alikuwa safarini, mwezini!
Hivyo hatukuonana. Tukawa tunawasiliana tu kwa simu na mbaya zaidi baba Princess alikuwepo nyumbani.
Nahisi ni mchanganyiko wa uchovu wa safari ya mwezini (if you know what am saying) pamoja na kero za baba Princess katika kukorofishana mama Princess akamjibu vibaya baba Princess. Baba Princess akaanza kujisifu kuwa angempata wapi mwanaume mwingine handsome kama yeye? Kwa hasira mama Princess akatoa simu yake na kumuonesha baba Princess picha yangu na kumwambia ajilinganishe kama anafikia hapo na kwamba ninampa zaidi ya yeye baba Princess anavyoweza kumpa. Sifahamu zaidi ya hapo ila najua baba Princess alimpiga sana mama Princess juzi ile. Akamtaka amuoneshe ninapoishi au kufanya kazi (hajui ninaishi karibu tu na kwake).
Asubuhi yake mama Princess akanitumia whatsapp message kuniambia niangalie nyendo zangu kwani baba Princess ananitafuta kwa udi na uvumba.
Kwa bahati nzuri nilikuwa njiani kuelekea Zimbabwe kusimamia uchaguzi hivyo nikawa nimepona, ila kwa sasa nipo njiani kurudi nyumbani. Pindi mtakapoona sionekani jukwaani mjue baba Princess kaniondoa duniani.
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
NB: Mke wa mtu sumu, ila mtamu kama asali (...sina maana hiyooo)!!!
No comments:
Post a Comment