Saturday, September 7, 2013

Postinor: Morning After Pills



Postinor-2 tablets

Postinor-2 is an oral emergency contraceptive. It may help to prevent a pregnancy if taken within 72 hours of unprotected sexual intercourse or failure of a contraceptive method.

Keep the drug out of the reach of children.

30th August 2007, Thursday

Niliripoti chuoni UDOM kwa ajili na kujiunga na masomo yangu ya juu ya shahada ya kwanza ya sayansi ya kompyuta. Kusema kweli sikuwa nimefikiri kama siku moja ningekuja kujiunga na chuo hiki kwani kama ilivyo ndoto ya wanafunzi wengi, nilitamani na mimi kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Moyoni bado sikuwa nimekubali hali ile ila nilijua njia pekee ya kunifanya niyamalize masomo yangu vyema ni kuanza kukipenda chuo kile. Na ukweli ni kwamba, licha ya maneno ya watu ya nje, ni chuo kinachojitosheleza na kina level sawa ya ubora wa elimu na chuo hicho cha Mlimani. Sadly, hili nimekuja kuligundua baada ya kumaliza chuo.

Masomo yalianza wiki moja baadaye na kuanza kusahau yale manung’uniko niliyokuwa nayo juu ya chuo.  Miaka miwili ilikatika haraka licha ya masomo kuwa magumu. Ni kozi ambayo inakutaka muda wote uwe updated, muda wote uwe unasoma la sivyo kile kilichokuwa kipya jana kesho ni historia.
Na kwa sababu hiyo, mimi na social life tulikuwa kama binti na mama mkwe. Hatukupatana sana licha ya marafiki zangu wengi kunishawishi hata kuwa natoka mara mojamoja.

Mahusiano pia yalikuwa neno geni kwangu kwani pamoja na kubanwa na masomo, sikuwa nimeona binti mzuri  bado wa kuweza kunishawishi.

Haikuchukua muda mrefu…

Jumatano, January 28th 2009

Ilikuwa kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa na siku hii pia kulikuwa na mashindano ya Miss Dodoma ambayo yalikuwa yakifanyika  eneo la Kilimani. Sikuwa na kazi nyingi sana za kufanya hivyo ilikuwa rahisi kwa marafiki zangu kunishawishi kwenda nao Kilimani kusherehekea sikukuu yangu hii pamoja na kuangalia show ile ya mashindano ya Miss Dodoma.

Mida kama ya saa mbili hivi jioni tulikuwa tumeshafika eneo la tukio. Kulikuwa na live band ya Msondo Band wakiimba wimbo wao maarufu wa ‘Wanaume tumeumbwa, mateso, mateso, kuhangaikaa.’ Basi tukakaa pale tukingoja maonyesho yaanze.

Katika mizunguko ya hapa na pale maeneo yale ya Kilimani, nakumbuka nilikuwa nataka kutoka nje, mara ghafla likaingia kundi la wadada watano ama sita hivi. Katika wadada wale mmoja alinivutia macho yangu kwa ulimbwende wake. Hata uvaaji wake kiasi ulikuwa tofauti kidogo na wenzake. Alivaa jeans iliyoonesha vyema hips zake zilizochomoza in perfect shape (sio oversize kukera na sio ndogo kuboa) na sleeveless top (iliyoyashika vyema matiti yake yaliyosimama kama katoka kuvunja ungo) wakati wenzake walivaa kama wapo ‘Ohio Street’. Na sura yake ya upole…vyote hivi nilivinotice ndani ya sekunde chache za wao kutembea kuingia eneo ambapo onyesho hilo lingefanyika. Ikanibidi nisimame kwa muda na kusahau kilichokuwa kinanitoa nje kwa wakati ule hadi kuhakikisha nimeona walipoenda kukaa.

Kwa ishu kama hizi kunahitajika timing ya maana. Wale experienced wanajua demu akiingia sehemu kama hizo hutakiwi kumkimbilia muda huo. Unaacha kwanza wajinga washoboke wee wanunue pombe then ndo unaingia, that way unakuwa ushamsoma yupoje na umepunguza gharama za pombe.

Mimi kwa ushamba wangu wa maeneo yale (lakini zaidi ni ulimbwende wa binti Yule) nikageuza njia kuelekea walipoketi wadada wale.

Mentor nikamfuata Yule dada moja kwa moja na kumgusa bega “Mambo?”

Dada: (akawaangalia wenzake kwanza kabla hajaitikia) “Tunafahamiana?”

Mentor: “Hapana ila nmekuona ukiingia pale nikavutiwa na wewe”

Mara ghafla akadakia rafiki yake, “Sasa unamsalimiaje mtu midomo mikavu? Mchukue ukamnunulie kinywaji ndo ustaarabu bana”

Mh! Sikuelewa kwanza. Wenzake nao wakaitika kama kumuunga mkono tena wakimnyanyua mwenzao anifuate. Yule binti kwa aibu kiasi akanyayuka hapo ndipo nikajua lengo lao maana walianza kutaja oda zao kama vile walikuwa wamempatia fedha. In total nlinunua redds moja ya Yule mrembo, konyagi mbili na Safari Lager nne. Nikapiga moyo konde kwani ukitaka cha uvunguni sharti ubinue kitanda.

Nikanunua vinywaji pale wakapelekewa wale wenzake na mimi na huyu mrembo (Dorah) tukakaa zetu pembeni, wakati huo show imeshaanza, tukaanza kufahamiana. Kwa usiku ule nilifahamu kuwa Dorah alikuwa mtoto wa mchungaji kwao Shinyanga, mtoto wa Kisukuma (ahem...), anasoma CBE pale pale Dodoma.

Moyoni nilifurahi kufahamu yale machache juu yake na nilipata shauku ya kufahamiana naye zaidi. Tukabadilishana mawasiliano pale na tukaendelea ku-enjoy show. Mida ilipofika nikajiunga na wenzangu tukarudi zetu chuoni.

Muda uliendelea kusonga na mimi na Dorah tulizidi kufahamiana. Ilikuwa ngumu kuonana mara kwa mara kutokana na umbali wa vyuo vyetu lakini tulikuwa tukiwasiliana kwa simu mara nyingi. Maisha na masomo yalisonga mbele…

Tukiwa mwaka wa tatu nilimwambia Dorah hisia zangu kwake na kwamba ningependa uhusiano wetu uwe more than friends. Nilikuwa nimempenda. Nikahisi labda angefaa kuwa mke wangu hasa kutokana na upole wake tuwapo pamoja. Kwa bahati nzuri alikubali akaniambia ananipenda pia.

Kumbe…

Kutokana na umbali wa vyuo vyetu na ukaribu wa CBE na viwanja vya kujirusha kuwa karibu na kwao mambo mawili yalijitokeza.

Moja, hatukupata muda mwingi wa kuonana au kuwa pamoja hasa nyakati za wikiendi. Kama sio masomo basi ataniambia yeye yupo bize au ana test mara assignment na mambo kama hayo alimradi kwa mwezi tunaweza tusionane kabisa na mara nyingi alisisitiza yeye kuja UDOM, sikuhisi lolote baya.

Pili, ilikuwa rahisi yeye kwenda kujirusha maisha club, club 84, kilimani bila mimi kujua ilhali nimeshaambiwa ana test jumatatu. Na kwa kuwa sikuwa mtu wa kujirusha basi alikuwa na uhakika sitokaa kuonana naye.

Maisha yaliendelea hadi nilipomaliza chuo 2010 na kurudi Dar es salaam kufanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya BIMA.

2011, January 28, Friday

Ni kumbukumbu yangu tena ya kuzaliwa. Siku hii aliniambia angekuja mapema asubuhi kuwa na mimi tusherehekee pamoja.

Kabla ya hapo, alikuwa amekaa kimya kwa kama wiki tatu hivi. Nikimpigia simpati, meseji hajibu na marafiki zake hawanipi jibu linaloeleweka.

Basi mida kama ya saa sita alifika Dar akitokea Dodoma. Nikaenda kumpokea kama mke wangu mtarajiwa kwa furaha zote. Ukweli akilini nilijua nimempata mke na baada ya mwaka mmoja atakapokuwa amemaliza chuo tuanze michakato ya harusi tuachane na dhambi ya kuzini. Unajua tena mtoto wa mchungaji na mkishazoea kufanya lile tendo hata condom mnaona inawaharibia starehe, kinachofuata mimba!

Fast forward to Usiku…

Jioni tulikuwa out na marafiki zangu hivyo we just enjoyed. Kama kawaida yake alikunywa redds moja tu na mimi nilikuwa nimeshazoea hivyo kwamba wala si mnywaji ni ile tu ya kishkaji. Nakumbuka rafiki yangu Shabani aliniuliza mbona demu wangu anaonekana mlevi sana anashangaa amekunywa redds moja tu. Mimi wala sikushtuka kwani kama si upofu wa mapenzi basi ni ushamba wangu.
Mida ilipofika tukaondoka zetu kurudi kwangu. Hapa ndipo drama ilipoanzia.

Tumefika vizuri ndani nikaingia kuoga tena nakumbuka nilimtania kumwambia, “Babes leo utansamehe mimi natangulia kuoga najihisi kunatanata sana. Ladies first tutafanya nkishamaliza.” Akacheka nikaingia bafuni.

Nilipotoka nikamkuta na yeye ameshajifunga khanga tayari kuingia bafuni. Mimi nikarudi chumbani nikawa nimekaa tu na pochi yake ikiwa imefunguliwa ipo juu kitandani. Ghafla nikaitupia macho nikaona kikaratasi kimejiotkeza kwa juu. Sikudhani kama kingeweza kuwa na madhara yoyote hivyo nikajinyosha na kukichukua na kuanza kukisoma;

Postinor-2 is an oral emergency contraceptive. It may help to prevent a pregnancy if taken within 72 hours of unprotected sexual intercourse or failure of a contraceptive method.

Nikahisi huenda yupo katika siku za hatari hivyo alipanga kutumia vidonge hivyo kuepusha mimba isiyotarajiwa. Lakini..au hapana..au..lakini, mbona siku zote huwa tunatumia kinga tu..postinor ni ya nini? Nililibrush lile swali pembeni baada ya yeye kutoka bafuni.

Tukaingia kitandani kupumzika na kama kawaida tulianza na kupasha kabla ya kuanza mechi. Baada ya kila mmoja kuwa tayari kwa mtanange nikajinyosha kuchukua buti zangu tayari kwa kuanza mechi. Akanikataza kuzivaa, nikamwambia, ‘lakini babe sitopenda yatokee tusiyoyapanga. Na nimeshaona vidonge vya postinor hivyo tusijiingize kwenye risk.’

Kwanza alishtuka kujua nimeona vidonge vile. Akataka kunikasirikia but nikamwambia isiwe tatizo yote hayo si tunafanya kujilinda, hakuna haja ya ku-panic. Aligoma kabisa kutumia condom akasema kama ni hivyo tusifanye.

Naishukuru roho iliyoniingia kukataa kufanya bila kinga. Tukalala ila hakulala kwa amani. Asubuhi akaenda kuoga na mimi kutokana na curiosity nikatamani kujua vidonge vile vikoje, vinafanyaje kazi na nini. Hivyo nikachukua kile kibox na kukifungua. Kwanza nikashtuka kukuta vidonge vinne tayari havipo ilhali karatasi yake imeandikwa ni vidonge vya kutumia baada ya tendo lenyewe.

Baada ya kutoka kuoga akaniambia hawezi kukaa tena anaondoka kurudi Dodoma. NIlimhoji kwa nini haraka vile akatoa visingizio vya assignment na nini. Sikutaka kumzuia sana nikaona nimuache. Nikampeleka Ubungo kama saa tano hivi akaondoka zake.

Baada ya kama wiki nne au tano hivi nikasikia kutoka kwa rafiki yake kuwa Dorah anaolewa.

Sikuelewa kwanza kwani tangu aondoke siku ile hatukuwasiliana sana na hata nikimpigia simu alikuwa ananijibu ki-shortcut sana. Kwa kweli nilipata shida kuelewa ni kwa nini ndipo nikamwomba rafiki yake, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa Dar, tukutane anielezee kisa na mkasa.

March, 2011…Posta

Aisha, rafiki mkubwa wa Dorah tulikutana EMS asubuhi mida ya chai kabla sijaingia kazini akaanza kunihadithia kuhusu rafiki yake.

Alianza kunisimulia;

Afadhali ndugu yangu hukukubali kungia kwenye mtego. Unajua Dorah wewe hukumfahamu kabisa hata robo yake. Tulivyokuwa chuo alikuwa mlevi balaa. Zile redds moja moja alizokuwa akinywa wakati mko pamoja zilikuwa geresha maana alijua umeshamuangukia hivyo asingependa kukupoteza mwenyewe alikuita husband material wake.

Hivyo alikuwa na wanaume wake wengi tu ndiyo maana ilikuwa shida wewe kuonana naye maana karibia kila weekend alikuwa out. Kwa kuwa wewe UDOM mbali na alijua si mtu wa kujirusha hakuwa na wasiwasi kama ungeweza kufumania nyendo zake. Hali ambayo ilionesha mafanikio hadi ulipomaliza na kuondoka Dodoma.

Tabia yake iliendelea hadi alipompata Kabezi, anayefanya usalama wa taifa. Mkaka Yule alikuwa na fedha za kutosha anahonga bila mawazo na kwa kuwa hakuwa mtu wa kukaa Dodoma sana ilikuwa rahisi kwake kuingizwa kwenye mtandao bila kijujua anachezewa pata potea.

Alikolea sana kwa mkaka Yule na kama kawaida mazoea yakishazidi matumizi ya kinga yanakosa maana. Hivyo katika mojawapo ya siku hizo ndipo Dorah aliposhika mimba. Kwa akili yake alijua akitumia Postinor (vidonge hivyo vya uzazi) maisha yataendelea kama kawaida kwani alishazoea na si mara moja tu kufanya vile.

Za mwizi arobaini. Siku ya siku alitumia postinor zake ila baada ya kama wiki mbili akapima akakuta ana mimba tayari. Postinor haikufanya kazi. Ndipo ikatokea kama bahati kwamba ilikuwa karibu na birthday yako hivyo lengo lake lilikuwa aje kwako akutegeshee then akusingizie mimba ni yako. Ghafla ukagoma ndipo aliporudi tukamshauri tu ambambikizie jamaa yake mwingine wa palepale Dodoma, muuza chips, mapema ili awapunguzie aibu wazazi wake hasa baba yake, mtoto wa mchungaji Yule maskini.

Hivyo ndo tuko kwenye maandalizi ya haraka haraka mwanaume mwenyewe hana mbele wala nyuma baba mkwe ndo anapanga harusi nzima anaolewa mwezi huu mwishoni.”

03 September 2013, Dodoma

Nimekuja Dodoma kikazi kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendelea. Sasa jana wakati naenda kuongeza mafuta kwenye gari nikakutana Dorah, bado mrembo ingawa lile tabasamu lake na uangavu wake umepotea kabisa. Alikuwa kambeba mwanae wa kiume wakielekea sokoni.

Tuliongea mengi sana akaniambia kuwa alikuja kuachwa na Yule mkaka pia baada ya kugundua mtoto si wake maana mtoto alitoka copyright ya Kabezi. Kwa sasa kaajiriwa kwenye ofisi ya @Bishanga kama secretary hivyo kidogo inamsaidia kusogeza siku.

Nimemkumbuka sana Dorah wangu usiku ila nikashukuru sana Mungu kwa kuniepushia janga lile. Anaonekana karekebishika ingawa ni baada ya kufunzwa na dunia.

Kikao cha leo cha bunge kimeniboa nikaona niwasimulie mkasa huu unaoelezea kwa nini @mentor mwenzenu bado nipo nipo sana.

Wasalaam wapendwa,
Mentor.

No comments:

Post a Comment