Thursday, July 3, 2014

Mimi ni Polisi: Fastjet


 30 June 2014

Ama kweli wahenga hawakukosea waliposema, ‘Ng’ombe wa masikini hazai. Akizaa hufaa. Asipokufa basi dume. Kama jike, tasa!’ Leo nimeugundua ukweli wa huu usemo.

Jumamosi, 07 July 2012 …Mitaa ya Mwenge Mwenge

Kwa askari Polisi, suala la kutokuwa na siku ya sikukuu ni jambo la kawaida kabisa. Siku hii nilipangwa zamu ya ukaguzi mida ya mchana maeneo ya Mwenge.Baada ya kumaliza kukagua malindo yote ya mchana kama inipasavyo kuwajibika. Nilikuwa katikati ya kutoa ripoti ya malindo hayo kwa mkuu wangu wa kituo. Ghafla…

Nilimsimamisha askari aliyekuwa akiendesha gari na nikazima radio call kwa muda (nitajibu hii kesi baadaye..ndivyo nilivyowaza kichwani). Nilishuka haraka kwenye gari na kuelekea kule nilipoona kile kilichonivutia.

“Samahani dada naomba kukusemesha kidogo” Nilijikuta nimeshamtamkia maneno hayo binti niliyemsimamisha. Kwanza alishtuka maana kusimamishwa randomly na Polisi kibongobongo sio ishara nzuri. Aliniangalia juu mpaka chini kasha kushusha pumzi baada ya kujihakikishia sina nia ovu kwake.
“Naitwa Afande Mentor (huku nikimuonesha jina langu lililoandikwa upande wa kulia mwa shati langu ‘E. E. Mentor’)’”

“Naitwa Winnie!” Bado alionekana kuwa na wasiwasi.

Kikweli sikumbuki yaliyoendelea pale ila nakumbuka kumweleza maneno ambayo kwa kawaida mtu angetumia robo saa ila mimi nilitumia dakika si zaidi ya nne. Mwisho wa siku tulibadilishana namba za simu na kuondoka. Nilimpigia tena mkuu wa kituo na kuomba radhi kuwa tuliona tukio ikabidi tukalishughulikie kwa haraka, ila ni minor na hakuna dhara lolote lililotokea. Askari dereva tuliyekuwa naye (mtu mzima kidogo kuliko mimi) aliishia kutingisha kichwa asiamini kilichotokea.

Winnie alinivutia sana nilipomuona. Katoto kazuri kabisa. Sikutaka kumuonesha hilo mapema ila tuliendelea kuwasiliana kwa kipindi kile na hata kuja kuwa marafiki wazuri tu. Kwa wakati ule ndio alikuwa ameanza kazi kampuni moja ya vinywaji hapa Dar. Haikupita muda mrefu sana na mimi na Winnie tukawa wapenzi. Ahaha aliniambia alivutiwa sana na jinsi nguo zangu zilivyokuwa zimenipendeza tofauti na mapolisi wengine anaowaonaga barabarani. Nilikuwa nimetupia shati langu la maboresho, nadhifu kabisa lililonoshika vizuri na viatu vyangu vimeng’arishwa mpaka unaweza kujiona.

Maisha yalikuwa mazuri.

Mwaka 2013 Septemba Winnie alipata kazi mkoani Mwanza na ilimbidi kuhamia huko. Ilikuwa ngumu kwetu kwani ilikuwa mwanzo sana wa penzi letu. Ila tulijiapiza kujaribu na kujitahidi kufanya penzi letu lidumu na kuendelea. Mawasiliano yalikuwa ndiyo kitu ambacho kilituweka pamoja. Na kwa hilo liliwezekana ingawa marafiki zake (ok, na zangu pia) walikuwa wakitukatisha sana tamaa.

Kwa upande wangu sikuwasikiliza kabisa wote walioniambia kuwa huko aliko anachepuka, au ana mtu mwingine kwa hiyo na mimi nitafute wa kupoozea wakati tunaendelea kuwasiliana. Alikuwa pia akiniambia hayo yalikuwa yakimtokea pia kwa upande wake na nilimtia moyo kuvumilia.

March, 2014

Mentor: “Good morning sunshine”
Winnie: “Good morning darling, how are you”
Mentor: “Am good and not so good”
Winnie: “Why, what’s wrong dear?”
Mentor: “I miss you badly”
Winnie: “ooooowh! Thanks d...I miss you too, you know!”
Mentor: “I do! I do! I just can’t help it though”
Winnie: “Haya bana…ila tumeonana juzi tu over your birthday”
Mentor: “Yeah…but that was way back in January!”
Winnie: “By the way, I could come over during sabasaba, si kutakuwa na long weekend!”

Yes! Yes! Yes! Nilifurahi kusikia vile na mara moja nilimweleza kuwa nitalishughulikia hilo. Tulikubaliana nifanye booking ya Fastjet kwa ajili ya yeye kuja Ijumaa asubuhi ya tarehe 04/07 na kuondoka tarehe 07/07 jioni. Gharama zake kwa fastjet zilikuwa considerably low. Kwa kamshahara kangu ka upolisi ningeweza kabisa kulifanikisha hilo na baada ya kufanya booking nilimweleza kuwa kila kitu kipo tayari. Aliniahidi kuongea na supervisor wake ili aruhusiwe kutokwenda ofisini hiyo Ijumaa na alikubaliwa.


Fast forward, 29th June 2014…Jumapili, 1835hrs

Kutokana na mechi ziendeleazo za mashindano ya kombe la dunia ratiba yangu ya kuongea na bebi Winnie ilibidi ibadilike. Nilikuwa nikmpigia kabla ya mechi za saa moja na tena kabla ya mechi za saa tano. Jana, nilimpigia jioni saa kumi na mbili hivi. Kwanza hakupkea simu hivyo nikasema ntampigia tena simu mechi itakapoisha. Na ndivyo nilivyofanya.

Mentor: “Hey D tsup!”
Winnie: “Hey”
Mentor: (nikaguna maana niliitikiwa flatly) “How’v u been? Umeshindaje?”
Winnie: “Mentor, I have something to tell you…I can’t make it to Dar hiyo tarehe 04”

Dah nilijihisi kuchoka. Ka laki mbili kangu nilijibana nikakata tiketi za fastjet – NON REFUNDABLE – mbona kanayeyuka hivi hivi? Ratiba zangu nilizozifuta kwa minajili ya kuspend wikiendi yangu na mpenzi wangu Winnie! Lakini kwa nini?

Nilimbembeleza sana Winnie aniambie nini hasa sababu ya yeye kushindwa kuja ila kila kisingizio alichokuwa akikitoa hakikuwa na mashiko. Baada ya kuongea kwa muda mrefu na dakika zangu za YATOSHA kwisha nilikata tamaa na kuamua kukata simu nijiandae kuangalia mechi ya saa tano usiku. Hata hivyo sikuwa nikiiangalia kwani suala la Winnie kuahirisha safari bila kuwa na sababu maalum ilinipa wasiwasi.

Huwezi nilaumu kwani niliwaza labda umbali umekuwa tatizo, hivyo uvumilivu umemshinda. Lakini kwa nini wakati huu ambapo ndio alikuwa karibu kuja kuonana nami? Niliwaza labda amekutana na mtu mwingine na tayari keshaangukia katika mtego wake. Niliwaza na kuwazua lakini sikupata jibu.

30th June 2014…facebook status ya rafiki yake Winnie

Vaileth Shirima (20TH June 2014): “Wanaume wengine sijui wapoje! Kama huna hela kaa na masikini wenzako wasio na sura na shepu! Mwanaume huna hela unakazana kutaka kumhudumia Miss Tanzania…utaweza wapi!?? Unajifanya upo romantic unanibukia ndege za wanuka shombo mwaka kabla. Kama upo romantic nipigie simu leo niambie ‘babe nimekukatia ticket ya saa moja jioni jiandae uje Dar nina hamu na wewe!’#Kantangazeeee

Nilikuwa napitia pitia facebook ndipo nilipokutana na ujumbe huu ulioandikwa na rafiki wa mpenzi wangu. Mwanzo sikuuelewa lakini baada ya kuendelea kumbana Winnie anieleze ukweli ndipo aliponifungukia kuwa, ‘marafiki zake wamemshawishi akatae kuja kwani sijawa romantic kisa nimembukia ndege miezi mitatu kabla badala ya kukata tiketi Alhamisi yeye asafiri Ijumaa’

Kwa kweli nimekosa cha kumjibu. Hadi sasa sielewi. Pesa yangu imepotea hivi hivi na Winnie ndo kaamua kuniacha kisa ushauri wa mashosti. Sikatai ni mzuri, lakini nilifanya vile kutokana na upendo wangu kwake na kuendana na uwezo wangu…

Wasalaam wapendwa,
Mentor.

No comments:

Post a Comment