Rafiki yangu…
Wakati nikiendelea kutafakari mustakabali wa mdogo wangu wa mwisho
ambaye tayari ameshakwenda Form five na kusahau machungu ya matokeo yao
halafu wanaambiwa mitihani imefutwa itasahihishwa tena.
Nilijua si wote waliofeli ni kwa sababu ya maisha ya siku hizi ya watoto kuwa facebook
muda wa vipindi kwani yeye namfahamu sana. Anapenda kusoma sana ila
matokeo yale hayakuwa sahihi….anyway, hilo si la leo bado nalitafakari.
Katika tafakuri zangu nikajikuta nimefika MUHAS...famously known as MUHIMBILI. Hapo napo kuna mdogo wangu, Vivian, yuko mwaka wa nne pale akisoma shahada yake ya kwanza ya udaktari.
Basi tukatoka for lunch and while there ndipo aliponielezea story ya rafiki yangu, Victor. Hata sijui kama bado nastahili kumuita rafiki.
Victor na Mimi
Mimi na Victor tumetoka mbali. Kwanza tulikuwa majirani hivyo michezo ya utotoni tuliicheza pamoja. Tumesoma wote tangu O’level kule Agape Lutheran Junior Seminary..tukarudia
wote mitihani ile ya 1998. Nakumbuka walikuwa wakiniita MCHUNGAJI. We
were still friends mpaka A’level tukaenda wote Moshi Sec. We were still
buddies tukapangiwa wote chuo yeye akaenda UDSM kusoma BCOM mimi Ardhi
University kusoma Architecture. He used to come home na akawa
anafahamika. Wadogo zangu wote walikuwa wanamheshimu na kumpenda kama
kaka.
Baada ya hapo mi nkaenda zangu Dodoma kufanya kazi nayeye akarudi Moshi kuendelea na biashara za wazazi wake.
September 2010
Mwaka huu Victor alijiunga na Masters program
tena palepale UDSM. So kama family friend nkamwambia afadhali upo Dar
kuna mdogo wangu yupo Muhimbili utakuwa unamcheki na yeye ajisikie kama
ana kaka. Akakubali.
So nikampa namba za simu za mdogo wangu…woe unto me!!!!
Fast forward to Friday, 2nd May 2013
Nimekuja Dar kufuatilia kitabu changu ninachoandika na kukifanyia printing pale UDSM Printing Press.
So nikampigia mdogo wangu simu kama yupo free. Akaniambia ndo ametoka
cadaver practical na hana tenda kipindi. Nikamwambia nampitia
anisindikize UDSM.
Safari yetu baada ya kumaliza kufuatilia kitabu na logistics zingine ikatufikisha Brajec kula. Ni hapo ndipo aliponipa stori ya Victor, my friend.
Ilianza kwa kumpigia simu usiku na kumtumia vocha. Vivian akaona ni jambo la kawaida..si ni kaka kanitumia? Siku nyingine anakuja
kumsalimia Muhimbili pale anamuuliza kama ameshakula au bado. Mara nyingi alikuwa akimwambia ameshakula hasa kwa sababu ya ratiba ngumu ya shule asingeweza kutoka. Maana kila weekend Victor alikuwa anakuja kumsalimia..what a brother!!!!!!!!!
Siku moja weekend kama kawaida Victor akaja kumsalimia halafu akamuuliza kama ameshakula nay eye akasema
bado. Akamwambia twende tukale. Akaingia kwenye gari haooooo…kushtukia
yuko Sinza…bar si
bar…Kelele..pombe nyingi…hakuna chakula kuna nyama tu..ikabidi waagize
tu nyama. Eventhough dogo anasema alikuwa na njaa kweli.
Shida ikaja kwenye drinks. Victor akaagiza Safari zake na mdogo wangu akaagiza Sprite. Mhh..akaanza
kumlazimisha anywe hata amarula sijui na nini. Hapo ndo dogo akashtukia
ameingia mkenge leo. Lakini huyu si ni kaka yetu jamani? Mbona anageuka
tena? Mara hataki kukaa mbali nay eye so akasogeza kiti karibu yake.
Mara aweke mkono wake begani mwake..aah alimradi shida tupu. Muda
unazidi kukatika. Victor anazidi kulewa..nyama haziji..kelele…njaa na usumbufu wake vilianza kunikera.
Ngoja nijiweke kwenye viatu vyake kwanza niendelee kuhadithia…kuanzia sasa Vivian (mdogo wangu) ndo anahadithia…
Alikuwa na ki-pimple chini
ya kidevu halafu kwanza alikuwa ameshakipasua. Akaniambia nikipasue.
Nikamwambia angoje kiive tena ndo akipasue akikipasua tena kitakuwa
kidonda. Mara ananing’ang’aniza nikipasue. Akamwita na waiter amletee
tissue. WTH..nikamwambia …Victor unapoteza muda wako tu siwezi kufanya kitu kama hicho.
Nikaona hapa ameshaanza kulewa hatutaelewana. Nikamwambia anirudishe chuo. Na nikamwambia, “Victor, next time you want to take me out, don’t bring me to such places. I hate noisy places and I prefer real food” Akasema, “I know the right place.” Tukaondoka ikabidi nibebe nyama zangu bila kuzila.
Kwa sababu ya giza lile sikujua tunaenda wapi ila nkashtuka tupo outside
Makumbusho. Nilikasirika sana yani nikamwambia nataka kwenda chuo sio
hapa. Eti akashuka kwenye gari akaenda kula minyama yake nje. Mi nkabaki
ndani namuangalia tu anavyokula vibaya kama nguruwe. Kwanza
hajanawa..anashika nyama na limkono lote..yani alinkera sana ile siku.
Akaingia ndani ya gari na mamikono yake michafu anaendesha huku anataka
kunishika mkono..yuuuuuuck!!! yani ikabidi nijifanye kila saa niko
kwenye simu tena nimeishika na mikono yote ili tu asinshike.
Akanirudisha chuo..nikashuka haraka sana tena wala hata sikumuambia asante wala nini. Nilimshusha hadhi sana ile siku. Nakumbuka neno lake la mwisho ile siku lilikuwa, “Dogo nimeupenda msimamo wako” Na tangu ile siku hajawahi kunipigia wala nini.
Ndo marafiki zako hao….
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
No comments:
Post a Comment