Tuesday, May 13, 2014

Mentor Utaoa Lini...?

Mentor utaoa lini…
2008, January 28 Jumatatu
Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu. Nilikuwa ninatimiza miaka 26. Kijana mtanashati nina miaka miwili kazini katika kampuni moja ya vinywaji.
Siku hii bosi wangu alinipa ofa ya kreti zima la vinywaji. Wafanyakazi wengu waliandaa sherehe ya kushtukiza kwa ajili yangu. Kwa kweli sikuwa nimeitegema kwani 'birthday' yako ikiangukia Jumatatu (kama ya mwaka huu) huwa huna mipango yoyote mikubwa kwani unajua siku inayofuata unahitajika kazini!

Nilipotoka kazini mshkaji akanipigia simu;
Mike: “Oya Mentor upo wapi?”
Me: “Dah ndo natoka kazini mtu wangu naenda nyumbani tu”
Mike: “Aaah pitia hapa NISIKUONE NA MWANANGU pub bana kuna mshkaji anasema anajua 'biometric readers' vizuri labda anaweza kukusaidia project yako”
Me: “Mh kaka, hatuwezi kukutana mwisho wa wiki?”
Mike: “mshkaji mwenyewe si wa kukaa sana kama vipi pitia tu si ndo njia hiyo hiyo ya kwenda nyumbani kwako?”
Basi bana mbele ya teknolojia, nisingeweza kukataa. Ikabidi na uchovu wangu nijikongoje hadi pale.


NISIKUONE NA MWANANGU Pub, 1830hrs
Ile naingia tu..nasikia SUUURRRRRRPPPPPPPRRRRRRRRIIIIIIISSSSSSSSEEEEEEEE!!! Ndo nikashtuka aaah kumbe ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu…Nilishangazwa kwa kweli ila nilifurahi sana...Tulikunywa sana pombe siku ile.

Kuna kitu kingine cha ziada kilitokea...nilikutana na msichana.

Binti mzuri sana kwa kweli. Miaka 25. Alikuwa anamalizia Shahada yake ya kwanza ya udaktari chuo cha Muhimbili.

Nadhani kwa sababu ya kinywaji nilichokuwa nimeshapata awali, nilipata ujasiri wa kumfuata nikaomba kucheza naye na alikubali.

Basi kidogo kidogo tukaanza kupiga hadithi za hapa na pale na hata muziki ulipoisha tukaenda pembeni kuendeleza mazungumzo. Aliniambia kuwa alikuja pale na dada yake ambaye ni mfanyakazi mwenzangu. Basi nikachukua mawasiliano yake tukawa tunaendelea kuwasiliana.

To cut the long story short…
Kidogo kidogo tulizoeana na ilichukua miezi miwili tu kuhakikisha amekuwa wangu. Alionesha kunipenda kwa dhati na hata alipomaliza chuo nilimwambia nataka kuanza michakato ya kumfanya awe mke wangu. Alinijibu sentensi ambayo kwa kipindi kile sikulitilia maanani, “Hilo tulishalijua!”

Basi michakato ya kwenda kwao ilianza nikamtumia mshkaji wangu Mike kwa kuwa alikuwa amenizidi anisaidie kufanya hiyo michakato ifane. Kama kupeleka barua na taratibu nyingine.

Nilimvalisha pete ya uchumba (ambayo alisisitiza aichague yeye kutoka kwenye duka la sonara alilolitaka yeye) na tukawa tunasubiri siku ya harusi tu tuhalalishe mambo.

2010 January 23 Jumamosi
Alikuja kwangu Ijumaa. Tukaenda kuangalia live band ya kina Hamis Mwinjuma kisha ikambidi aje kulala kwangu aondoke asubuhi awahi kazini kwani alikuwa zamu siku hiyo.

Basi kwa haraka ya kuwahi kazini asubuhi ile akasahahu simu yake kwangu. Mida kama ya saa tatu hivi nilishtushwa na mlio wa simu. Nilijua haikuwa simu yangu kwani simu yangu siku zote huwa haina mlio (ringtone). Nilifuatiliza mlio wa simu na kuikuta chini ya mto aliokuwa ameulalia. Alikuwa akipiga shoga yake mmoja hivi. Iliita kama mara tatu na nilipoona anaendelea kupiga, ilinibidi niipokee tu.

Nikapokea;
Shosti: “We mwanga wa kike nikipiga mimi unajifanya upo na jianaume lako ambalo kama sio mimi usingelipata. Muone kwanza na leo nina maagizo toka kwa mganga wako nimeamua nikuambie kwa mdomo si unajifanya kusoma message hujui!

Ilinibidi nikate simu kwa mshtuko. Hamu ya kutaka kujua zaidi iliniingia, ikanibidi niingie ndani ya simu ambayo kwa muda wote wa mahusiano yetu sikuwahi kuigusa. Nakumbuka kuna kipindi niliishiwa dakika za kupiga ghafla ikabidi nimuombe nimpigie mshkaji akanitaka nitaje namba aandike mwenyewe na nilipomaliza akataka kukata mwenyewe.

Nikazama kwenye ujumbe wa maneno…
Nilishtuka sana siku ile. Sikujua kama haya mambo bado yapo, mambo ya kwenda kwa waganga? Binti mrembo vile? Na kanisani mbona alikuwa anakwenda? Na usomi wake je? Nilijiuliza mambo mengi sana nikakosa jibu.

: kulikuwa na masharti ya kuhakikisha ananipata na ninakuwa mumewe kwa hali yoyote ile
: kulikuwa na masharti ya kuhakikisha anapata pesa kama kuvaa chupi moja kwa mwezi
:kulikuwa na masharti ya kuendesha gari bila kuvaa chupi
:kulikuwa na masharti ya kulala juu ya kaburi (hizi ni siku aliniambia anaenda safari za kikazi, semina, au anafuatilia usajili)

Nimekuwa peke yangu tangu wakati huo…

Wasalaam wapendwa,
Mentor.

No comments:

Post a Comment