Tuesday, July 2, 2013

Nataka Kupima

NATAKA KUPIMA… (inspired by Diamond's - Nataka kulewa)
Ayayayaya….
We niache niende..niende niende….


Usiniulize kwanini sababu utanizingua, ukitaka jiunge na mimi mara ya mwisho ni lini we ulipima
Mi mwanzo sikuamini nikajuaga siezi ukwaa, kumbe mjinga ni mimi nayekula maganda meyatoa.

Oh uzinzi…uzinzi ulinifanya Muumba nikamzoea vibaya
Mi siezi pitisha hata siku bila kumuona Tina
Oh uzinzi…uzinzi ulinifanya Muumba nikamzoea vibaya
Na nina wengi ah..nimewapitia peeku.

Nataka kupima (PIMA)
Mi nataka kupima (PIMA)
Nataka kupima (PIMA)
Nikikutwa nianze dozi!!!!!


Ayayayaya….
We niache niende..niende niende….


Mi kwa uzinzi tajiiri, nkajivisha na taji la ubingwa
Sijali vimini-mini, ama wageti wanaofugwa ntawaomba
Kumbe wenzangu na mimi ni bure tu nlijisumbua
Wengine kama ishirini waliomba wakapewa na kavu wakagonga.

Oh uzinzi…uzinzi ulinifanya Muumba nikamzoea vibaya
Mi siez pitisha hata siku bila kumuona Tina
Oh uzinzi…uzinzi ulinifanya Muumba nikamzoea vibaya
Na nina wengi ah..nimewapitia peeku.

Nataka kupima (PIMA)
Mi nataka kupima (PIMA)
Nataka kupima (PIMA)
Nikikutwa nianze dozi!!!!!


Ayayayaya….
We niache niende..niende niende….kupima..kupima…


Wasalaam wapendwa,
Mentor!



NB:
Nimekaa nikafikiri, nimekuja kugundua WE ONLY LIVE ONCE..but if you live it right, ONCE IS ENOUGH. Nisingependa mwingine aje kuimba huu wimbo kama mimi.

Jitafakari…then jiulize, “NATAKIWA KUPIMA?” Nafsi ikikataa kwenda jiambie tu moyoni, “Ah, namsindikiza Mentor”..then, CHUKUA HATUA!!!!!

No comments:

Post a Comment